Jumatano 22 Aprili 2026 - 09:56
Umadhubuti wa Lebanon na shinikizo la Iran vilisababisha kusitishwa vita

Hawza/ Kamal al-Khair, mkuu wa “Kituo cha Kitaifa Kaskazini mwa Lebanon”, amesema: Lau si shinikizo la kila siku la Iran wakati wa mazungumzo, pamoja na umadhubuti wa Lebanon katika kukabiliana na jeshi la adui wa Kizayuni, basi vita visingesitishwa hata kidogo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Kamal al-Khair, mkuu wa “Kituo cha Kitaifa Kaskazini mwa Lebanon”, alisisitiza kwamba; Serikali ya Lebanon imeendelea kuwapa kipaumbele na nyadhifa rasmi watu wasiofaa; watu ambao hawakuweza kubeba wajibu wa kitaifa waliokabidhiwa.

Aliongeza kuwa; jukumu lao lilikuwa ni kuilinda nchi yao na watu wao na kutokukubali mashinikizo ya Kizayuni Marekani. Hivyo basi, ni muhimu katika hatua ijayo kufanyiwa kazi uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa inayojumuisha nguvu zote na kuzingatia maslahi ya umma, kwa kuwa hatua ya sasa inahitaji msimamo wa pamoja, kinyume na maamuzi yanayochukuliwa leo na mamlaka ambayo yako kinyume na matakwa ya wananchi.

Al-Khair alieleza kwamba; mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika mjini Washington D.C. kati ya balozi wa Lebanon nchini Marekani na balozi wa utawala wa adui kwa upatanishi wa Marekani ni “mkutano wa aibu”; kwa kuwa ulifanyika sambamba na kuendelea kwa uchokozi mkubwa dhidi ya Lebanon na kuuawa na kujeruhiwa kwa maelfu ya watu kutokana na makombora ya Kimarekani ambayo jeshi la adui linayatumia kulenga maeneo mbalimbali ya Lebanon.

Mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Lebanon pia alisisitiza umuhimu wa msimamo wa kitaifa wa Nabih Berri, ambao ulikuwa ni nguzo kuu ya umoja wa kitaifa uliojitokeza wakati wa vita na ambao umeendelezwa leo kupitia taarifa yake.

Al-Khair alibainisha kwamba; amani ya ndani na umoja ni mipaka myekundu, na kila aina ya kuvunja nguzo hizi mbili—kutoka upande wowote ule—ni kushambulia uwepo wa Lebanon na ni zawadi ya bure kwa adui wa Israel na mipango yake; mipango ambayo inaweza kufanikiwa tu kupitia kuchochea fitna.

Alisisitiza kwamba; lau si shinikizo la kila siku la Iran katika mchakato wa mazungumzo—pamoja na sharti la kutorejea katika mazungumzo hayo isipokuwa baada ya kusimamishwa kwa vita nchini Lebanon, jambo lililotangazwa pia na upande wa Pakistan—na pamoja na kusimama kishujaa uwanjani, hasa katika kukabiliana na jeshi la adui wa Kizayuni kusini na hususan katika mapambano ya kishujaa ya mji wa Bint Jbeil, basi kusingekuwa na kusitishwa vita hata kidogo.

Aliongeza kuwa: Wote wanajua kwamba, lengo kuu la adui lilikuwa ni kuiteka kikamilifu kusini mwa Lebanon, lakini mizinga na wanajeshi wake walishindwa mbele ya kujitolea kukubwa kwa wananchi na vikosi vya Muqawama ambao waliinywesha ardhi kwa damu yao safi.

Kamal al-Khair alitoa wito wa kujifunza somo kutokana na vita hivi; vita ambavyo Hizbullah iliviendesha kwa siku 45 na kwa kujitolea kwa vijana wake ilithibitisha kwamba, adui wa Kizayuni haelewi isipokuwa lugha ya nguvu. Hapa ndipo inapodhihirika ulazima wa kutumia kipengele kikuu cha nguvu ya Lebanon, yaani Muqawama na silaha yake; silaha ambayo leo ndiyo kizuizi pekee dhidi ya utekelezaji wa mipango ya adui nchini.

Al-Khair pia aliwasalimu wananchi wanaounga mkono Muqawama; wananchi ambao kwa kurejea haraka katika ardhi zao, kupuuza vitisho vya Kizayuni, kushikamana kihistoria na msimamo wa kitaifa, kuunga mkono Muqawama na kuwa tayari kujitolea kwa uwezo wote katika njia ya kulinda nchi yao, wamethibitisha kwa vitendo subira na uaminifu wao.

Katika ngazi ya kikanda, Al-Khair alisifu juhudi zinazofanywa na Pakistan, pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Uturuki na Misri katika kuimarisha umoja na uthabiti katika nchi za Kiarabu na Kiislamu, na akazitaka nchi hizi kuunda safu ya pamoja ya kukabiliana na mradi wa Kizayuni na Marekani; mradi unaolenga kudhibiti rasilimali za mafuta na maji za eneo hili na kulazimisha ajenda zake kwa mataifa ya Umma wa Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha